Wednesday, September 30, 2015

Anonymous

Kama Wewe ni Mtumiaji wa Twitter Basi Taarifa Hii Inakuhusu Sana!

Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu mtandao wa Twitter kuongeza idadi ya maneno ya kutweet kwa Tweet moja… kwa sasa Twitter inamruhusu mtumiaji kutumia uwingi wa maneno 140 tu kutweet message moja lakini kwa wale ambao wanapenda kuchat kwa marefu, Twitter iliamua kongeza idadi ya maneno kufikia 10,000 kwa private messages… je tutegemee mabadiliko yoyote hivi karibuni?
TWEET2
Nimekutana na habari muda huu ambayo ningependa kushare na wewe mtu wangu… inasemekana kuwa Twitter ipo kwenye mpango wa kuongeza idadi ya maneno ambayo mtu anaweza kuandika kwa Tweet moja na kwa mujibu wa mtandao wa http://www.complex.com Twitter ina mpango wakuleta huduma itakayowaruhusu watumiaji wake kutweet ama kuandika Tweets/post zenye maneno zaidi ya 140!
TWWET6
Baadhi ya mitandao kama Re/Code  wa Marekani wanaamini kuwa maamuzi haya yamesukumwa na mabadiliko ya idadi ya maneno ya kutumia kwenye private messages za Twitter>>> “watu wamepokea vizuri ongezeko la maneno ya Twitter kwenye message za private, hii inaonyesha jinsi gani ambavyo bado kampuni ina nafasi ya kukua zaidi ya hapa…” <<< mmoja ya wafanyakazi wa Twitter aliuambia mtandao wa Re/Code.
Je Twitter itaweza kukuza biashara yake katika ushindani wa Teknolojia na mitandao ya kijamii safari hii? Kama ilikuwa haijakufikia basi ichukue hiyo mtu wangu na pengine tutegemee kufaidika very soon na mpango huu!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.