Martha Mboma, Dar es Salaam
MBEYA City haitaki masihara hata kidogo kwani imeweka sheria kali inayokataza wachezaji wake kunyoa au kuweka mitindo ya nywele kama kiduku, rasta na mingineyo ili wawe ‘serious’ na soka tu.
Kutokana na sheria hiyo, miongoni mwa watakaoathirika ni kipa wake mpya Juma Kaseja aliyewahi kucheza Simba na Yanga, kwani kichwani amesokota ‘dread’ fupi.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, ameliambia Championi Jumamosi: “Sheria zetu zinafahamika na zinaeleweka siku zote lakini pia makubaliano yetu na mchezaji hamjui yapo vipi kama atatakiwa kufuata kanuni au laa lakini itategemeana katika hilo.
“Katika timu yetu, kitu cha kwanza tunachokipa kipaumbele siku zote ni nidhamu ndani na nje ya uwanja bila kuangalia nani ni nani ili kuweka usawa.”
Mbali na Kaseja, wachezaji wengine wa Mbeya City walioathirika na sheria hiyo ni Themi Felix na Juma Nyosso (dread) na Cosmas Fredy ‘Balotelli’ mwenye kiduku, wote wameshanyoa nywele zao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.