Tunaendelea kuelezea habari ya Mwanasiasa Zuberi Mtemvu aliyepingana na Mwalimu Nyerere kabla ya uhuru:
Kilichofuata
baada ya kupatikana uhuru mwaka 1961 ilikuwa ni kukamatwa, kuwekwa
kizuizini na kuhamishwa kwa baadhi ya wapinzani waliodhaniwa kuwa
wanapinga utawala wa Mwalimu Nyerere.
Miongoni mwa waliokamatwa ni Abdillah
Schneider Plantan, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh,
Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff
Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba na Shariff Adnan.
Wengine
ni Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdallah
Mwamba, Sheikh Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, Salum
Abdallah Popo, Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab
Kiguu cha Mbuzi na wengine wengi.
Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote
katika wale waliokamatwa na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa.
Baadhi yao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wakishirikiana na wale
waliodhaniwa ni wapinzani wa Mwalimu Nyerere.
Maalim
Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu walihusika na
Msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako Sheikh Hassan bin Amir,
wakati huo akichukuliwa kuwa ndiyo roho ya waumini wa Tanganyika,
alikuwa akiendesha madrasa yake kila magharibi pale msikitini,
kilichofanywa wakamatwe ni siri ya wana usalama.
Shariff Hussein na nduguye Mwinyibaba
walihamishiwa Kenya, walikotoka si kwa sababu ya Uislamu wao bali
Nyerere alielezwa kwamba walikuwa wamejishughulisha katika harakati za
kuipinga serikali yake.
Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa
kizuizini kwa sababu kila mara alikuwa akifuatana na Sheikh Hassan bin
Amir kama vile alikuwa kivuli cha sheikh. Kilichomfanya Nyerere kuwatia
kizuizini watu hao na wengine kuhamishwa ni kile kilichoelezwa kuwa ni
usalama wa taifa lakini Zuberi Mtemvu alisalimika.
Itaendelea wiki ijayo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.