Hamida Hassan, Gladness Mallya
Msanii wa filamu Bongo, Kelvina John
juzikati alifanyiwa bonge la pati na kigogo mmoja wa migodini
Bulyanhulu, Injinia Paulo Maira ambaye alimmwagia ‘mapesa’ na kumuahidi
ndoa ‘soon’ baada ya kumtolea mahari.
Pati hiyo ilifanywa maalum kwa ajili ya kumpongeza kwa kutimiza miaka
32 ya kuzaliwa ambapo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Jozi Lounge
‘Msasani Village’, Msasani jijini Dar.
Akizungumza kwa furaha kwenye pati hiyo, Kelvina alimshukuru Mungu
kupata mwanaume anayempenda ambaye amembadili kutoka kwenye maisha
f’lani na kuelekea kwenye ndoa.
“Mtarajie ndoa hivi karibuni kwani nimeshatolewa mahari jamani,
nimeamua kuolewa na wala sitarudi nyuma, unajua mtu kukukubali ukiwa
tayari na watoto wawili kwangu naona ni upendo wa hali ya juu,” alisema
Kelvina kwenye pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao.
Sherehe ikiendelea.
Kelvina akisaidiwa kukata keki.

Note: Only a member of this blog may post a comment.