STAA wa filamu za Kibongo
Jacqueline Pentzel maarufu kama Jack wa Chuz ametamba kuwa ndoa yake na
Gardner Dibibi ipo imara licha ya kukumbwa na misukosuko ya kuachana na
kurudiana.
Akiteta na gazeti hili hivi karibuni,
msanii huyo alisema kuwa hakwenda kucheza kwenye ndoa kama wasanii
wenzake wanavyodhani, kwani licha ya kumuombea mabaya, amemudu kuwa
imara kwa kumaliza matatizo yao kila yanapotokea na maisha yanaendelea.
“Ukweli wasanii wenzangu wamekuwa
wakiniombea kila kukicha ili niachike, lakini kwa hilo wameshindwa na
niwaambie tu ukweli kwamba sijaja kucheza segere kwenye ndoa kama wao
wanavyofikiri,” alisema Jack Chuz.

Note: Only a member of this blog may post a comment.