Jambo
lingine muhimu ni mwanamke kuchunguza idadi ya siku za mzunguko wake
mrefu wa hedhi. Toa siku 11 kutoka katika idadi ya siku za mzunguko huo
na utapata namba fulani.
Halafu tena anza kuhesabu katika
mzunguko wako ujao wa hedhi kwenda mbele hadi kufikia siku ambayo una
uwezekano wa kupata mimba. Kwa mfano iwapo mzunguko wako mrefu ni siku
31, toa 11 katika mzunguko huo na utapata 20.
Iwapo hedhi yako ijayo inaanza Oktoba 3,
ongeza siku 20 kuanzia siku hiyo na Oktoba 23 itakuwa siku yako ambayo
una uwezekano mkubwa wa kubeba mimba.
Kwa utaratibu huo utakuwa umepata
kipindi cha kati ya Oktoba 14 hadi 23 ambacho ni siku ambazo una
uwezekano mkubwa wa kubeba mimba au Ovulation window kitabibu.
Ovulation huweza kubadilika kidogo
katika mzunguko wako wa hedhi kwa sababu Ovulation huweza kucheleweshwa
na sababu mbalimbali kama vile wasiwasi au fikra nyingi, ugonjwa, lishe
au kufanya mazoezi.
Kipindi cha Ovulation kinaainisha siku za kubeba mimba?
Kipindi cha kubeba mimba huanza siku 4
hadi 5 kabla ya Ovulation, na humalizika saa 24 hadi 48 hii ni kwa
sababu muda wa Ovulation huweza kuchelewa au kuwahi kutokana na sababu
mbalimbali.
Pia kwa sababu mbegu ya kiume huwa na
uhai kwa siku 4 hadi 5 na yai huweza kuishi kwa masaa 24 hadi 48 baada
ya kuingia katika tumbo la uzazi.
Hivyo kwa kujua siku hizo humsaidia
mwanamke kufahamu kipindi chake cha Ovulation kimewadia na hivyo kuweza
kukutana na mumewe au mwenza wake wakati huo ili aweze kubeba mimba.
Mambo ya kufanya ili kupata ujauzito haraka
Leo tunaangalia jambo la kufanya ili mwanamke aweze kupata mimba.
Mwanamke unapaswa kuufahamu mzunguko wako wa siku za mwezi vizuri.
Mzunguko wa siku zako za mwezi utakusaidia kufahamu ni siku gani yai lako linakuwa limepevuka.

Note: Only a member of this blog may post a comment.