Wednesday, September 9, 2015

Anonymous

Hili Ndio Jiji la Dar! Hakika UKISTAAJABU ya Musa Utayaona ya Firauni Hapa! Shuhudia Vijana Wanavyoharibika Hapa...

OFM (4)-001Deogratius Mongela na Chande Abdallah
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni! Wakati Jeshi la Polisi Tanzania likitoa semina mbalimbali kwa wananchi kuhusiana na ulinzi shirikishi, hali si shwari kabisa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar kutokana na uuzwaji wa pombe haramu aina ya gongo, Risasi Jumatano linakupasha.
Mara kwa mara serikali imekuwa ikikemea uuzwaji wa pombe hiyo inayowainua mabega wanywaji ‘makenchi’ ambapo askari wamekuwa wakijitahidi kuzuia kwa nguvu zao zote, lakini bila matokeo mazuri.
OFM (1)-001Jumatatu iliyopita, makamanda wa kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers walipata malalamiko kutoka kwa  wakazi wa eneo la Ubungo jijini Dar waliosema uuzwaji wa pombe hiyo haramu umewaathiri kiafya vijana wa eneo hilo kiasi cha kushindwa kufanya kazi za ujenzi wa taifa na kujiingizia kipato.
Ilibidi OFM ifike katika maeneo yaliyotajwa na kuchunguza kwa kina ili kuupata ukweli wa madai ya wakazi hao ambao wengi ni wazazi au walezi.
OFM (2)-001“Jamani mje huku Ubungo au Manzese muone vijana walivyochakazwa kwa gongo. Wembambaaa! Wamechongeka! Hawana nguvu. Hii pombe ni sumu, itaangamiza taifa jamani,” alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo bila kujitambulisha jina.
Maeneo yaliyotajwa kukithiri kwa kuuzwa gongo na ambayo baadhi ya vijana huanza kunywa pombe hiyo tangu asubuhi ni Ubungo ya Urafiki, Manzese, Mabibo, Manzese ya Tip Top na eneo la Ubungo Maziwa.
Katika uchunguzi wa OFM, ilibaini kuwepo kwa biashara hiyo katika vilabu vya pombe maeneo hayo ambapo pombe hiyo huuzwa kama vinywaji vya kawaida haswa katika maduka madogo yanayouza vyakula pamoja na vibanda maalum vinavyouza vileo vya kisasa.
OFM ilijionea uuzwaji wa pombe hiyo ukiendelea ambapo biashara hiyo ni ya kipekee kwani watu maalum ndiyo wanaouziwa kwa kuogopa kugundulika.
Hata hivyo, taarifa zilizotua katika dawati la OFM zilidai kuwa, wauzaji hao hushirikiana na baadhi ya walinzi wa serikali bila kukamatwa kwani huwapoza kwa kitu kidogo.
Siku hiyo, OFM nao walijifanya kama wateja kwa kuwatumia watu maalum ambao ndiyo hutumika kwenye dili hilo na kufanikiwa kuuziwa kadiri walivyohitaji.
OFM walifika katika kila eneo husika ambapo walitakiwa kutoa kiasi cha shilingi elfu moja, baada ya kutoa pesa hiyo wakasubiri kwa muda wa takribani dakika tano wakaletewa kinywaji hicho kilichohifadhiwa kwenye chupa za maji safi lakini huku muuzaji akitokea eneo ambalo mnunuzi hawezi kulijua.
Hata hivyo, baadhi ya maeneo, OFM walishtukiwa na wauzaji hao kutokana na kutokuwa na mwonekano wa wanywaji wa gongo waliozoeleka ambapo karibu wote wana afya dhaifu.
“Aaa! Msela, wewe siyo bwana! Nimeghairi sasa, hatuuzi gongo hapa,” alisema muuzaji mmoja maeneo ya Ubungo ya Urafiki na kukimbia na chupa yake baada ya kumbaini kamanda wa OFM kuwa hakuwa ‘taipu’ ya wateja wake.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.