WAJUMBE 310 wa Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata), leo wakiwa
mkoani Dodoma wamemchagua Sheikh Abubakary Zubeir kuwa Mufti wa Tanzania
akiziba nafasi iliyoachwa na hayati Issa Shaaban bin Simba.
Kabla ya uchaguzi huo, Sheikh Abubakary Zubeir, alikuwa Kaimu Mufti
wa Tanzania kwa kipindi cha mpito baada ya kifo cha Sheikh Mkuu, Issa
Shaaban bin Simba.
Awali Sheikh Zubeir alikuwa Naibu Mufti wa Sheikh Mkuu na pia Mjumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa nchini.

Note: Only a member of this blog may post a comment.