Shani Ramadhani
Kampeni zinaendelea vizuri katika kila upande na hata yale maneno
yanayoongelewa ni utani kama ule uliop kwenye timu za mpira wa Yanga na
Simba, changamoto kubwa iliyopo ni kwa wapiga kura kwa sababu wanatakiwa
kuangalia sera muhimu kama afya na elimu kutoka kwa wagombea wao.
Kwangu naona muelekeo wa kampeni ni mzuri lakini tunaomba hali ya
amani na utulivu iwe hivi hivi mpaka siku ya uchaguzi itakapofika ili
tupate kuchagua viongozi sahihi watakaotuwakilishia matatizo yetu huko
bungeni.
Muonekano wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu uko vizuri sana tu sema
wanatuharibia wale watu wanaotumia muda huu kutoa kauli chafu zenye
kuwakera watu badala ya kutangaza sera muhimu kwa wananchi kwa sababu
wao ndiyo waamuzi.
Kampeni za mwaka huu ni tofauti na za miaka iliyopita kwa sababu
kuna muamko mkubwa kutoka kwa akina mama na vijana ambao wengi wao wana
kiu ya kupata mabadiliko na hata idadi ya wapiga kura nayo inaonekana
kuwa kubwa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.