KAatibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel
Na Gladness Mallya
KATIBU Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella
Joel amesema kifo cha mumewe Yeronimo Mwalo ni pigo kubwa kwake
linalohitaji maombi ya kila siku.
Akizungumza kwa huzuni, Stella alisema mumewe alifikwa na umauti
Ijumaa iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alilazwa kwa
muda wa siku nne akisumbuliwa na uti wa mgongo.
“Kweli nimepigwa jamani, nahitaji tu maombi maana peke yangu siwezi,
nilikuwa nimemzoea mume wangu, nilimpenda lakini Mungu amempenda zaidi,
ukweli naumia,” alisema Stella.
Mwili wa marehemu Mwalo uliagwa Jumatatu katika Kanisa la Pentekoste
Light House lililopo Ubungo, Dar na kusafirishwa kwenda katika Kijiji
cha Mbiwili, Iringa na kuzikwa jana Jumanne.
Note: Only a member of this blog may post a comment.