Wednesday, September 23, 2015

Anonymous

Haya ni Maneno 15 ya LOWASSA na 26 ya ZITTO KABWE, Baada ya TWAWEZA kusema CCM inakubalika 66 %

Kuelekea uchaguzi mkuu October 25 2015 matokeo ya utafiti wa taasisi ya TWAWEZA yametolewa September 22 2015 Tanzania na kuonyesha Watanzania mbalimbali wanamkubali nani zaidi ambapo CCM imepata 66%, CHADEMA ikipata 22%, C.U.F 1%, ACT 0%, NCCR 0%, UKAWA 3%.
Baada ya utafiti huu kutoka chumba cha habari kilipitia page za Twitter za Wagombea Urais na vyama vyao kutazama kama kuna walichoandika baada ya kupata haya matokeo. 

Mgombea Urais Edward Lowassa ambaye yuko kwenye tiketi ya CHADEMA ameyaandika haya kwenye page yake halali ya Twitter >>> ‘Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki, tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata
Dr. Magufuli hakuwa ameandika chochote kuhusu utafiti huu huku tweet yake ya mwisho ikiwa inaeleza furaha yake kwa jinsi Wananchi wa Bukoba walivyojitokeza kumsikiliza.
Kwa upande wa ACT Wazalendo, kiongozi wake Zitto Kabwe aliandika kwenye Twitter ‘Chama chetu kinaamini kwenye tafiti haijalishi zina matokeo mazuri au mabaya kutuhusu, tumepokea matokeo haya kama changamoto… tutaongeza nguvu yetu kuhakikisha tunapata asilimia zaidi kwenye kura’ 

Kingine alichosema Zitto ni >>> ‘Ikumbukwe kwamba utafiti huu wa TWAWEZA umefanywa kabla ya chama cha ACT WAZALENDO hakijapata mgombea Urais na kabla ya uzinduzi vilevile
January Makamba wa CCM kwenye sehemu ya Tweets zake aliandika kwamba hajashangazwa na matokeo ya utafiti wa TWAWEZA sababu imeendana na utafiti na CCM ambao ulitangazwa siku chache kabla.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.