Msanii wa filamu aliyetamba kwenye Bado Natafuta, Gabo Zigamba
amesema filamu yake mpya ‘Safari ya Gwalu’ italeta mapinduzi nchini.
Gabo ameiambia Bongo5 leo kuwa uwezo aliouonesha katika kazi hiyo utawafanya watu waamini kipaji chake.
“Mimi nategemea mafanikio makubwa kwa sababu hii ni miba ya nyikani
na haivunjiki kwa mkono,” amesema. Ajira isiyo rasmi sasa tunakwenda
kuirasimisha, lazima nifanye vitu ambavyo vitaleta mapinduzi na
changamoto kwa wengine. Safari ya Gwalu ni filamu inayokwenda kuishi kwa
muda mrefu kwa sababu ni sinema ambayo itarudisha safari ya Gabo.”
Amesema filamu hiyo itatoka September 28.
-via Bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.