Monday, September 7, 2015

Anonymous

FAHAMU KUHUSU UVIMBE KWENYE OVARI KWA MWANAMKE-4


Nikukaribishe mpenzi msomaji katika ukurasa huu wenye elimu ya kukupa ufahamu juu ya afya zetu. Kwa wiki kadhaa tumekuwa tukipeana elimu juu ya uvimbe katika ovari za mwanamke. Tumeangalia aina za uvimbe pia tukaangalia dalili za mwanamke mwenye tatizo hili la uvimbe kwenye ovari.

Leo ningependa tuangalie madhara ya uvimbe huo kwa mwanamke mjamzito.
Tatizo la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke wakati wa ujauzito pia hutokea. Mara nyingi wanawake wajawazito wenye uvimbe kwenye mayai yao huwa na uvimbe ambao siyo saratani.
Madhara ya uvimbe kwenye mayai wakati wa ujauzito

Uvimbe kuwa mkubwa sana na hivyo kusababisha maumivu makali kwa mjamzito, kama uvimbe huu utapasuka au kujinyonga wenyewe (twist on itself), basi kuna uwezekano wa mimba kuharibika hivyo kutoka(miscarriage) au kujifungua mtoto mapema zaidi (pre- term labor).

Kupasuka kwa uvimbe huu hakuleti madhara ya maambukizi yoyote yale.
Uvimbe huu ukiwa mkubwa na kujinyonga wenyewe au kukandamiza mfuko wa kizazi na hivyo kukandamiza kiumbe kilichomo ndani yake. Mwanamke mjamzito atahitaji upasuaji ili kuondoa uvimbe huu. Upasuaji hautamuathiri mama wala kiumbe kilicho ndani ya tumbo. Lakini kama unavyojua, wakati wa upasuaji kunaweza kutokea madhara yoyote yale, hivyo mwanamke mjamzito mwenye uvimbe kwenye mayai hushauri wa kuepuka upasuaji kama anaweza.

Kama uvimbe huu utahitaji kufanyiwa upasuaji ili uondolewe, muda mzuri wa kufanyiwa upasuaji kwa mwanamke mjamzito ni kuanzia wiki ya 13-28 ya ujauzito wake.Uvimbe mdogo huweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji ya Laparascopic surgery kama nilivyoeleza hapo juu, kwa uvimbe mkubwa, utahitaji kuondolewa kwa kufanyiwa upasuaji kwenye maeneo ya tumboni.

Kutokana na uvimbe mkubwa kwenye mayai ya mwanamke kuwa na madhara mengi, mwanamke mjamzito atahitaji uangalizi wa karibu kutoka kwa daktari.Kama mwanamke mjamzito mwenye uvimbe kwenye mayai yake atatimiza miezi tisa ya ujauzito wake bila matatizo yoyote, anashauriwa ajifungue kwa njia ya upasuaji ili wakati wa upasuaji uvimbe ule nao pia uondolewe ili kumuepusha kufanyiwa upasuaji tena.

Kwa kuwa uvimbe huu huwakuta hata wajawazito wanaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu kwa wajawazito ambao hupata maumivu makali kutokana na kupasuka kwa uvimbe huu. Pia matumizi ya dawa za usingizi wakati wa kujifungua kwa mwanamke mjamzito mwenye uvimbe kwenye mayai yake bado ni salama.

Nakushauri msomaji wangu ufuatilie kwa makini makala haya ili kujua vizuri kuhusu tatizo hili.
Lakini kama una tatizo hili na unajisikia aibu kumweleza mwenzi wako tupigie simu katika namba zetu au tutembelee Sigwa Herbal Clinic katika vituo vyetu vilivyopo Dar es Salaam, Mbeya, Njombe, Singida, Kahama, Moshi, Morogoro, Dodoma, Arusha, Tanga, Kigoma, Mwanza.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.