Wednesday, September 9, 2015

Anonymous

ESTER KIAMA: BADO NINA IMANI NA CCM

ester-kiama

Msanii wa filamu Bongo, Ester Kiama.
Gladness Mallya
MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Ester Kiama amefunguka kwamba bado ana imani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuiongoza nchi kwani kinao uwezo wa kutatua matatizo ya wasanii.
Akichezungumza na gazeti hili, Ester alisema anaipenda CCM na anamsapoti mgombea wake wa urais, Dk. John Magufuli na kuwataka Watanzania wote kuungana naye kwani anaamini chama hicho kikishinda kitafanya mabadiliko makubwa tofauti na miaka mingine. 

“Naomba CCM ipewe nafasi tena, naamini mabadiliko makubwa yatakuwepo, hata sisi wasanii tutaondokana na matatizo yanayotukabili kwani hali ni mbaya sana kwa sasa kwa sababu filamu hazipokelewi tena kwa Mhindi, hivyo tupo tu ndiyo maana wengi wameamua kuingia kwenye siasa,” alisema Ester.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.