Mtoto wa kike wa H.Baba, Tanzanite, amedaiwa kutajwa kushiriki katika mashindano ya urembo ya watoto wa mastaa nchini Rwanda.
H.Baba ameiambia Bongo5 kuwa hivi karibuni Tanzanite atasafiri kuelekea nchini Rwanda kwaajili ya mashindano hayo.
“Kenya tayari wameshamuona, mwezi wa 12 anaenda Rwanda kwenye
mashindano ya urembo ya watoto wa mastaa ambayo yanafanyika nchini
Rwanda,” amesema H.Baba. “Tanzania kachaguliwa Tanzanite peke yake.
Kwahiyo sisi wazazi tumefarijika kupata mtoto ambaye ana bahati na ana
nyota ya kupendwa.”
-via Bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.