Msanii wa muziki, Baracka Endrew
‘Baracka De Prince’ amefunguka kuwa kufuatia skendo iliyokuwa
inamkabili ya kutoka kimahaba na Video Queen maarufu Afrika, Agness
Gerald ‘Masogange’ ameamua kujiweka naye kando mdogomdogo ili kuepusha
maneno kutoka kwa wambeya.
Akichonga na Ijumaa
juzikati, Baracka alisema anajua watu wanahisi ‘anabanjuka’ na ‘mtoto’
huyo kutokana na ukaribu wao hivyo ameona ni vyema afanye liwezekanalo
ili kuondoa mawazo hayo kwa watu.
“Kiukweli yule wala siyo demu wangu na
kwa kuwa huwa sipendi manenomaneno yasiyokuwa na ukweli, nimeamua
kupunguza ukaribu na Masogange na hata picha zake nyingi Instargram
nimefuta na yeye nilimwambia afanye hivyo akakubali,” alisema Baracka.

Note: Only a member of this blog may post a comment.