Friday, September 11, 2015

Anonymous

ALI KIBA Aisaliti YANGA SC, Aungana na SIMBA!

Ali Kiba nzuri_full
Wilbert Moland, Dar es Salaam
MKALI wa muziki wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wa Chekecha Chekecha, Ali Kiba, jana aliingilia msafara wa timu ya Simba kwenye Uwanja wa Ndege wa Tanga kisha kupiga picha na baadhi ya wachezaji wa timu hizo. 

Kiba ambaye inajulikana wazi ni shabiki ‘damu’ wa Yanga, alikutana na msafara huo dakika chache baada ya wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo kutua jijini hapo wakitokea Zanzibar saa tisa alasiri.
Akiwa uwanjani hapo, msanii huyo alionekana mwenye furaha baada ya kukutana na wachezaji hao wakiwemo Waganda, Simon Sserunkuma na Hamis Kiiza.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.