Watu tisa wamejeruhiwa huku magari na pikipiki zikiharibiwa baada ya
kutokea vurugu zilizohusisha wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwenye kampeni
jijini hapa.
Tukio hilo lilitokea juzi katika eneo la Mbata, kata ya Ghana ambapo mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CCM, Sambwee Shitambala, alipokuwa akifanya mkutano wa hadhara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alithibitisha tukio hilo kuwa wakati Shitambala akiendelea na mkutano, ulijitokeza msafara wa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Mr. Sugu na kupita katika eneo hilo kuelekea eneo la Nsowo, hali iliyosababisha mtafaruku.
Alisema baada ya msafara huo kupita katika njia hiyo ambayo ilikuwa ikikatiza pembezoni lakini jirani kabisa na mkutano wa mgombea wa CCM, wafuasi wa vyama hivyo walianza kushambuliana kwa kurushiana mawe.
Polisi walipopata taarifa walifika haraka katika eneo hilo na kukuta vurugu zikiendelea, lakini walifanikiwa kuzizima ingawa tayari watu tisa walikuwa wamekwishajeruhiwa na magari mawili, moja la CCM na lingine la mgombea ubunge wa Chadema Sugu, yaliharibiwa kwa vunjwa vioo, alisema.
Aliwataja waliojeruhiwa katika vurugu hizo kuwa ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Robert Kerenge (58), Salum Mwansasu (35), Atupele Brown (39), Sakina Salum (25) na Maranyingi Matukuta (31), wote wafuasi wa CCM.
Wengine ni Agabo Mwakatobe, mkazi wa Ghana na Jailo Mwaijande (23), mkazi wa Itiji, wote wafuasi wa Chadema pamoja na Gabriel Mwaijande ambaye ni dereva wa Sugu.
Kamanda Msangi alizitaja mali zilizoharibiwa katika vurugu hizo kuwa ni gari la Mbunge anayemaliza muda wake, Mbilinyi aina ya Toyota Land cruiser VX lenye namba za usajili T 161 CPP ambalo lilivunjwa kioo cha mbele, taa moja ya nyuma upande wa kushoto, na kioo cha upande wa dereva, pikipiki na gari moja la CCM lililovunjwa kioo cha mbele.
Kamanda Msangi alisema baada ya kutokea kwa vurugu hizo, wagombea wote wawili na baadhi ya wafuasi wao walihojiwa katika kituo cha polisi cha kati na baada ya kutoa maelezo waliachiwa. Kamanda Msangi alisema kuwa upelelezi kuhusu tukio hilo unaendelea na kwamba jalada la shauri hilo limepelekwa kwa mwanasheria.

Note: Only a member of this blog may post a comment.