Milango ya show za kimataifa inazidi kufunguka kwa vijana wa wanne
wanaounda Yamoto Band yenye maskani yake Temeke, Dar-es-salaam.
Ile ahadi aliyoitoa mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella
kupitia Bongo5 kuwa Yamoto Band wamepata mwaliko wa kwenda
kuwaburudisha Watanzania na wana Afrika Mashariki waishio Marakeni
imetimia.
Promota maarufu DMK ambaye amekuwa akipeleka wasanii wengi kufanya
maonesho Marekani, ikiwa ni pamoja na ile show ya Ommy Dimpoz na Shilole
inayotarajiwa kufanyika Septemba 5, 2015, ameshare poster ya show ya
Yamoto Band itakayofanyika katika jiji la Kansas Novemba 27, 2015.
Fella amesema kuwa wakiwa huko Yamoto wanatarajiwa kufanya show
katika miji mitatu. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Yamoto Band
kufanya ziara nchini Marekani.
-via bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.