Estela Melendez 91
Nimekutana na stori moja kutoka mji mdogo wa La Boca ulioko Chile ambako mwanamke wa miaka 91 amekutwa na mtoto tumboni ambapo mtoto ujauzito huo kaubeba kwa zaidi miaka 60.
Estela Melendez mwenye umri wa miaka 91 amekua akilalamika kwa zaidi ya miaka ishirini kwa kuwa na uvimbe mgumu tumboni mwake na hakuwahi kuhisi ana ujauzito na wala hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito.
Estela Melendez akiwa na baadhi ya ndugu zake
Baada ya madaktari kumfanyia vipimo na uchunguzi wa kutosha wamegundua ya kuwa mwanamke huyo alishika ujauzito akiwa na umri wa miaka 30 hivi, kitu ambacho kimewashangaza ndugu zake wengi ni kwamba yeye na mume wake waliambiwa hawawezi kupata watotoalafu leo zimekuja stori nyingine.
Estela Melendez amesema hakuwahi kuhisi dalili zozote kwa kipindi chote ila alijihisi uvimbe mdogo ukimuuma na kuacha kwa nyakati tofauti…alikuwa akipata maumivu mara mojamoja lakini zaidi ya hapo uvimbe huo umemkosesha raha kwa miaka mingi.
Hiki ndio kilichokutwa tumboni mwa Estela Melendez
Madaktari wamesema uvimbe huo hauna madhara yoyote kwa mwanamke huyo ila wanajianda kumfanyia upasuaji kuutoa uvimbe huo, kwa sasa Estela Melendez amelazwa hospitalini akisubiri kufanyiwa operation hiyo.
Nimekuwekea video hiyo hapa!

Note: Only a member of this blog may post a comment.