Thursday, August 6, 2015

Anonymous

Mastaa wa soka na vioja vyao Uwanjani>>Balotelli, David Luiz na Ibrahimovic na wamo…-PICHAZ

Wachezaji mpira ni miongoni mwa watu maarufu sana kutokana na kazi yao kupendwa au kuwa na mashabiki wengi kutoka sehemu mbalimbali, miongoni mwa vitu ambavyo huwezi kuvidhania kama unaweza kuviona kwa mastaa wako wa soka ambao umezoea kuwaona wakiwa katika muonekano uliozoeleka kuonekana labda wakiwa katika mechi au matukio ya kawaida.
Katika pitapita zangu mtandaoni nimekutana na hii list ya mastaa wa soka waivyoamua kujiachia kwa vioja kabisa.

Dani Alves

Dani Alves aliwahi kuvaa wigi wakati akisherehekea ushindi wa Timu yake ya Taifa

Andrey Arshavin

Ni mchezaji wa zamani wa Arsenal anatajwa kuwa sio miongoni mwa watu wanaouchukulia mchezo wa mpira wa miguu serious.. Ndani ya Uwanja akaona afanye kioja kupindisha uso wake.

Mario Balotelli

Chochote anachokifanya Balotelli huwa hakiko mbali na headlines za Waandishi wa Habari. 

Antonio Cassano

Antonio Cassano akishangilia ushindi wa goli 2-0 Italy ilivyoifunga Ufaransa katika michuano ya Euro 2008.
Zlatan Ibrahimovic

Zlatan Ibrahimovic wakati alipovua nguo Uwanjani bila hofu kabisa.
Stephen Ireland

Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester City Stephen akishangilia goli kwa staili ya kuvua bukta
David Luiz

David Luiz beki ghali wa klabu ya PSG ya Ufaransa akishangilia goli

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.