Thursday, August 20, 2015

Anonymous

Steve NYERERE Apata AJALI!

steve nyerereMCHEKESHAJI maarufu na msanii wa Filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ hivi karibuni amefungukia jeraha lake la usoni alilolipata katika ajali  alipokuwa njiani akitokea Dodoma kurudi Dar. 

Akizungumzia tukio hilo, Steve alisema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Chalinze Dodoma akiwa na gari lake binafsi aina ya Toyota Passo ambalo liliacha njia na kupinduka na kumsababishia aumie usoni huku wengine aliokuwanao garini kunusurika.
“Ilikuwa ajali mbaya kwa kweli, namshukuru Mungu kutoka salama, nilikuwa pamoja na vijana wangu lakini wao walikuwa salama kabisa mimi ndiyo niliumia hivi mpaka nikafikia hatua ya kushonwa nyuzi kadhaa usoni,”alisema Steve.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.