MASHARTI! Kanisa Katoliki limemzuia staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel kumbatiza mwanaye kutokana na kutokidhi matakwa ya kanisa.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni mara baada ya mwigizaji huyo
ambaye imani yake ni ya Kiislamu, kutaka kumbatiza mwanaye huyo ambaye
baba yake ( Moze Iyobo) ni Mkatoliki.
“Alikuwa amejipanga kumbatiza Kikristo kutokana na imani ya baba
mtoto wake lakini alipokutana na padri Paul Ruwaaich wa Parokia ya Uparo
Moshi aliyekuwa Dar kikazi akamtaka akaanzie kusali kwenye Jumuiya
Ndogondogo (mtaani kwake), abadilishe dini ndipo mtoto huyo abatizwe
kwani ndizo taratibu za Kanisa Katoliki.
“Alipopewa sharti hilo, lilikuwa gumu kwa Aunt, ikabisi ageuze zake,” kilisema chanzo chetu.
Mwanahabari wetu alipomuuliza Aunt kuhusu suala hilo, alisema amebaki njia panda na anatafakari cha kufanya.
Note: Only a member of this blog may post a comment.