Tuesday, August 25, 2015

Anonymous

KIMENUKA! Aliyewahi Kuwa Waziri, Lawrence Masha Ambaye Kwa Sasa Kahamia CHADEMA Akamatwa na Jeshi la Polisi!

Aliyekuwa waziri wa Mashauri ya Ndani ambae sasa ni mwanachama wa CHADEMA Mh Laurance Masha amekamatwa jioni ya leo na jeshi la polisi nchini.

Tukio la kukamatwa Masha limefuatia kukamatwa kwa wanachama 18 waliokuwa kwenye harakati za kawaida za uenezi wa chama chao katika kampeni ya kawaida ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ambayo haizuiwi na sheria yoyote ile nchini.

Baada ya kukamatwa vijana hao na kufikishwa kituo cha Ostarbay, Mh Masha aliamua kwenda kufuatilia sababu za kukamatwa kwa wanaukombozi hao, ajabu alipofika tu nae akatiwa mbaroni.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.