Meneja wa TMK Family pamoja na Mkubwa na Wanawe, Said Fella amesema
kuwa anatamani angepata nafasi ya kufanya kazi na muimbaji Barnaba japo
kwa miezi sita.
Fella ambaye amevumbua vipaji vya vijana wengi wa Temeke wakiwemo
Yamoto Band, amesema hayo katika post ya kumpongeza Barnaba aliyekuwa
akisheherekea siku yake ya kuzaliwa weekend iliyopita.
“Kuna vitu vya kulazimishwa lakini sio kuonyesha hisia mimi
msanii wangu katika madogo walio chipukia wakati mh JAKAYA mrisho
KIKWETE yupo madarakani ni uyu mwanangu barnaba mtoto wa kaka ruge
muttahaba wakati anakivumbua nilisema ili zao akubahatisha hii ni nguzo
moja muhimu ya kuta ya Tht na pia natamani boss ruge aniachie uyu kijana
miezi sita najua yatafanyika mapinduzi ya hatari Leo ana kumbuka siku
yake ya kuzaliwa happy birthday mwanangu barnaba mtoto wa kaka” aliandika Fella Instagram.
Mfano wa kile Fella anachotamani kukifanya kwa Baranaba, ni kama pale
aliposaini na Shaa na kumbadili kutoka kufanya muziki wa ‘kishua’ hadi
‘kiswazi’, na kutoa wimbo wa ‘Sugua Gaga’ ambao video yake hadi sasa ina
views 19,605,962 Youtube ambazo Shaa hakuwahi kuzipata katika video
zake zote zilizopita.
Tuesday, August 11, 2015
Natamani Nimsimamie Barnaba Hata Miezi Sita – Said Fella
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
WASANII
on Tuesday, August 11, 2015
Note: Only a member of this blog may post a comment.