Muimbaji wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo amethibitisha kuwa anakuja
nchini Kenya hivi karibuni kwaajili ya kushiriki kwenye kipindi cha
Coke Studio Africa.
Siku chache baada ya taarifa kusambaa kuwa Ne-Yo ndiye msanii wa
kimataifa atakayeungana na mastaa wa Afrika katika kipindi hicho mwaka
huu, ametumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuthibitisha ujio
wake.
Hii ni mara ya pili Ne-Yo anarudi Afrika katika kipindi cha muda
mfupi. July 18, 2015 alitumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA huko Durban,
Afrika Kusini.
Note: Only a member of this blog may post a comment.