Saturday, August 1, 2015

Anonymous

Mwinyi wa YANGA SC Haelewi Nini Kilitokea Kwenye Penalti

Beki wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi.
Hans Mloli,Dar es Salaam
BEKI wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi, juzi alijikuta akikosa penalti ya tatu na kupoteza dira ya Yanga kusonga kwenye michuano ya Kombe la Kagame, lakini mchezaji huyo amefunguka kuwa bado haelewi nini kilitokea siku hiyo wakati anapiga penalti ile.

Yanga ilifungwa kwa njia ya mikwaju ya penalti 5-3 na Azam FC katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Mwinyi ameliambia Championi Ijumaa kuwa, wakati anakwenda kupiga penalty, alijipanga na mpaka anafika kwa kipa, alikuwa tayari ameshampoteza kwa kumuangalia kwa macho lakini baada ya kupiga hali ikawa tofauti na ilivyotarajiwa.

“Yaani sijui ilikuwaje pale, kwa sababu napigaga vizuri tu penalti na hata ile pia nilikuwa nimeamini napata kwa kuwa nilishampoteza kipa lakini nashangaa aliirudia na kudaka lakini haikuwa penalti mbaya, sijui hata nini kilitokea,” alisema Mwinyi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.