Saturday, August 1, 2015

Anonymous

HABARI NJEMA YANGA SC: Mastaa Hawa Wawili Hatari Wapewa Ruksa Kutua JANGWANI!

Mshambuliaji, Michael Olunga.
Wilbert Molandi na Hans Mloli
UONGOZI wa Klabu ya Gor Mahia ya Kenya, umekubali kumuuza mshambuliaji, Michael Olunga na kiungo mkabaji, Khalid Aucho kwenye kikosi cha Yanga kwa masharti maalum.Wachezaji hao wametajwa kwenye usajili wa Yanga lakini bado kumekuwa na giza nene kwenye usajili huo.

Yanga, tayari imeanza mazungumzo ya kumsajili Olunga huku klabu hiyo ikisema ipo tayari kutoa dau la shilingi milioni 87.Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Gor Mahia, David Kilo, alisema Yanga kama wanataka wachezaji hao wasubirie Ligi Kuu ya Kenya imalizike ndiyo iwasajili, lakini siyo kipindi hiki.

Kilo alisema ni ngumu kuwaachia wachezaji hao katika kipindi hiki ambacho ligi kuu ya nchi hiyo inaendelea huku wenyewe wakipanga kutwaa taji hilo la ubingwa.Aliongeza kuwa ni vyema Yanga wakasubiria hadi ligi kuu ya huko itakapomalizika Novemba, mwaka huu ndiyo watue kuichezea Jangwani.

“Tumepata taarifa za Yanga kuwataka baadhi ya wachezaji wetu wenye mikataba, hivyo kama uongozi hatuoni sababu ya kuwaruhusu kuichezea Yanga kwa sasa, lakini kama watafuata masharti watawapata.“Moja kabisa, lazima wachezaji hao wamalize Ligi Kuu ya Kenya ndiyo watue kuichezea Yanga, kwa sababu ni ngumu kuwaachia wakati ligi inaelekea kumalizika na sisi tukihitaji ubingwa huo.

“Kama uongozi, tunawaomba Yanga kusubiria kwanza wachezaji hao wamalize ligi kuu ndiyo wajiunge na Yanga, lakini siyo katika kipindi hiki, ni vyema wakalifahamu hilo,” alisema Kilo.Kwa upande wa Aucho alisema: “Mimi sina tatizo lolote, ninawasikiliza viongozi wangu wa Gor Mahia, kuamua hatma yangu kutokana na kuwa na mkataba wa miaka miwili.”

Naye Olunga alisema: “Mimi nipo tayari kujiunga na Yanga, kikubwa wao ni kuwafuata viongozi wangu na kufanya mazungumzo nao.”Aidha, Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, alithibitisha kuvutiwa na wachezaji hao kwa ajili ya kuwasajili kwa kutamka kuwa ni wachezaji wazuri wanaostahili kuichezea timu hiyo.

“Yule kiungo mkabaji wa Gor Mahia anayevaa jezi namba 10 (Aucho), ni mzuri sana, ni aina ya wachezaji ninaowahitaji kikosini kwangu, ana uwezo wa kupiga pasi fupi na ndefu, hivyo anastahili kuichezea Yanga kama tukifanikiwa kumpata.

“Pia yule Olunga ni mshambuliaji mzuri sana na zaidi nimevutiwa na umbo lake kubwa tofauti na uwezo wake wa kufunga, anafaa kumtumia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Pluijm.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.