Saturday, August 1, 2015

Anonymous

MGOSI, KIIZA Waondolewa Kikosini SIMBA SC!

Mohammed Mdose,Dar es Salaam
KOCHA mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, ameweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna mchezaji ambaye tayari amejihakikishia namba kwenye kikosi cha timu hiyo.

Kocha huyo amesema hata wale mastaa kama Mussa Hassan Mgosi na Hamisi Kiiza, hawana uhakika wa kuwa kwenye kikosi chake cha kwanza hadi baada ya mazoezi ya wiki tano ndiyo atajua nani anaweza kucheza na nani hawezi.

Simba ambayo kwa sasa inaonekana kupania kurudisha makali yake kwenye ligi waliyoyapoteza kwa misimu mitatu iliyopita, imeamua kukaa kambini nje ya Jiji la Dar, baada ya kutoka Tanga katika kambi ya wiki mbili, kwa sasa wamejificha visiwani Zanzibar.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Muingereza huyo alisema kuwa tangu atue kuinoa timu hiyo mapema mwezi huu, mara kwa mara amekuwa akiziangalia ‘DVD’ za mechi za Simba zilizopita, hivyo anachokifanya kwa sasa ni kumjenga kila mchezaji ili aweze kufiti kwenye kikosi cha kwanza. Alisema ameamua kufanya hivyo ili kufuata falsafa yake aliyojiwekea ya kuiandaa timu yake kuwa fiti muda wote, hivyo atakayezubaa ataozea benchi. “Wiki tano kuanzia sasa kabla ligi haijaanza ndipo nitajua muelekeo wa timu yetu, nimewaambia wachezaji wangu kuwa kila mtu ana nafasi ya kuvaa jezi ya Simba na sitakuwa na kikosi cha kwanza cha kudumu, kwani timu inatakiwa kuwa na makali wakati wote.“Pia sitaki kuwa na wachezaji 11 tu waliojihakikishia nafasi ya kucheza,” alisema Kerr.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.