Saturday, August 1, 2015

Anonymous

Kocha wa SIMBA SC Awaponda YANGA SC!

Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr,
Richard Bukos, Zanzibar
KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, ambaye juzi Jumatano alikiacha kikosi chake kikiendelea na mazoezi kisiwani Zanzibar na kwenda Uwanja wa Taifa jijini Dar kushuhudia robo fainali ya Kombe la Kagame, kati ya Yanga na Azam, amesema Yanga ni timu ya kawaida sana.

Kocha huyo amesema anashangaa viongozi wake kumueleza kila siku kuwa aifunge Yanga wakati yeye anaiona ya kawaida sana.Akizungumza na Championi Ijumaa kwenye mazoezi yaliyofanyika jana asubuhi katika Uwanja wa Amaan, kisiwani hapa, Kerr alisema ameiona mechi hiyo na kusema si kwamba Yanga hawana wachezaji wazuri lakini Azam walifanya vizuri zaidi licha ya kwenda sare mpaka kufikia hatua ya matuta. “Kutokana na msisitizo huo, nimelazimika kufuatilia baadhi ya mechi za timu hiyo, nimeona mambo kadhaa lakini sioni la ziada katika timu hiyo nikiilinganisha na kikosi changu ambacho nasikia nitaletewa wachezaji wengine wa kimataifa kwa ajili ya kukiimarisha.“Yanga waliocheza juzi ni wa kawaida sana na hawatishi,” alisema Kerr.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.