Kila binadamu anapokuwa mdogo huwa na
malengo au ndoto yaani ni namna ambavyo angependa kuwa wakati
atakapokuwa mkubwa. Kila mtu utakayebahatika kukutana naye atasema mimi
nataka kuwa hivi na mwingine akasema ningependa kuwa vile, sio kila
ndoto au mipango tunayopanga huwa kama tulivyopanga.
August 5 nakuletea story ambayo team ya millardayo.com ilipata nafasi ya kumuuliza nahodha wa klabu ya Dar Es Salaam Young African na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Cannavaro yeye kipindi yuko mdogo alitamani kuwa nani ni kweli mpira ilikuwa ni ndoto yake?
“Hayo
mambo anakuwa anapanga mungu dream yangu mimi nilikuwa nataka kuwa mtu
wa kawaida tu niwe askari lakini kila kitu anapanga mungu hata kwenye
mpira nilikuwa napenda sana kuwa golikipa lakini nikawa central
defender”>>>Cannavaro
Cannavaro alijiunga na Yanga mwaka 2006 akitokea katika klabu ya Tembo Sports klabu ya kutokea kwao visiwani Zanzibar.

Note: Only a member of this blog may post a comment.