Friday, August 21, 2015

Anonymous

Majibu ya JAMES MBATIA Kuhusu Haya >> Uchaguzi na DK. SLAA, UKAWA Kuzuiwa Kutumia Uwanja wa Taifa…(Audio)

J MBATIA
James Mbatia ni mmoja wa Viongozi wa Umoja wa UKAWA, August 20 2015 amekutana na Waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Makao Makuu ya NCCR- Mageuzi, Ilala Dar. 

Kazungumzia kuhusu ishu ya UKAWA kuzuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwenye uzinduzi wa Kampeni zao, Uchaguzi na kutoonekana kwa Dk. Slaa. 
>>> “Kampeni zinaanza nawasihi Wanasiasa wote wachunge ndimi zao sana, tujadili hoja kwa hoja kwenye majukwaa ya kisiasa sio kujadili watu, matusi, wala kupigana ngumi au kumwaga damu… Tume ya Uchaguzi ambayo ndio refa itende haki pamoja na vyombo vya dola… Wakitenda haki hakuna mgogoro wa aina yoyote, Kamati za Ulinzi na Usalama Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hatutaki waingilie mchakato huu. 

Kuhusu kuzuiwa Uwanja wa Taifa Dar majibu yake ni haya>>> “Uwanja wa Taifa ni mali ya Watanzania, tutakutana tutatafakari alafu tukishakubaliana kwa pamoja tutatoa taarifa wapi tutakutana na tutazungumza nini, kwa kweli hatuna majibu mpaka sasa hivi“– James Mbatia. 

Haya ndio Majibu ya James Mbatia kuhusu ishu ya Dk. Slaa kutoonekana kwenye Vikao vya UKAWA >>> “UKAWA sio Mbatia, sio Slaa sio Lipumba sio Mbowe… tusijadili watu tujadili hoja za msingi za taifa, watu wanapita, tuzungumzie Watanzania zaidi
Sauti ya James Mbatia iko hapa chini, ukibonyeza play utamsikiliza kila alichokisema kuhusu hayo matatu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.