Tuesday, August 4, 2015

Anonymous

LIVE UPDATES: Yanayojiri katika Mkutano mkuu wa CHADEMA Ukumbi wa Mlimani City, DSM Leo!

Leo ni tarehe 4/8/2015 siku ya Jumanne.Ni alfajiri njema kabisa ambapo Taifa litasimama wakati likishuhudia mkutano mkuu wa CHADEMA mshirika wa UKAWA utakaokuwa na kazi moja kubwa ya kumpitisha mgombea pekee wa Urais kupitia CHADEMA na UKAWA.

Jina pekee mpaka sasa lililopitishwa na vikao vya juu ni la Kamanda mpambanaji Mzee wa maamuzi magumu Edward Ngoyai Lowassa. Jina hili ndilo litawasilishwa kwenye mkutano mkuu ili kupigiwa kura.

Waziri Mkuu huyo wa zamani anatarajiwa kutoa hotuba mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu na mbele ya Taifa.Hotuba inayotarajiwa kuwa mwongozo wa Tanzania tunayokwenda kuijenga kuanzia Oktoba.

Timu nzima ya wapashaji habari wa CHADEMA imepiga kambi usiku kucha hapa mlimani city ili kuwaletea kila kitakachojiri.Tunatarajia vituo kadhaa vya Televisheni kama ITV,Chanel Ten,Azam TV na radio kadhaa ikiwemo Radio One kurusha matangazo haya moja kwa moja kuanzia saa 5 asubuhi..
Karibuni sana hapa www.kandiliyetu.com usipitwe!
Ukumbi wa mlimani City unavyoonekana kabla ya wajumbe kuingia:

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.