Leo
ni tarehe 4/8/2015 siku ya Jumanne.Ni alfajiri njema kabisa ambapo
Taifa litasimama wakati likishuhudia mkutano mkuu wa CHADEMA mshirika wa
UKAWA utakaokuwa na kazi moja kubwa ya kumpitisha mgombea pekee wa
Urais kupitia CHADEMA na UKAWA.
Jina
pekee mpaka sasa lililopitishwa na vikao vya juu ni la Kamanda
mpambanaji Mzee wa maamuzi magumu Edward Ngoyai Lowassa. Jina hili ndilo
litawasilishwa kwenye mkutano mkuu ili kupigiwa kura.
Waziri
Mkuu huyo wa zamani anatarajiwa kutoa hotuba mbele ya wajumbe wa
mkutano mkuu na mbele ya Taifa.Hotuba inayotarajiwa kuwa mwongozo wa
Tanzania tunayokwenda kuijenga kuanzia Oktoba.
Timu
nzima ya wapashaji habari wa CHADEMA imepiga kambi usiku kucha hapa
mlimani city ili kuwaletea kila kitakachojiri.Tunatarajia vituo kadhaa
vya Televisheni kama ITV,Chanel Ten,Azam TV na radio kadhaa ikiwemo
Radio One kurusha matangazo haya moja kwa moja kuanzia saa 5 asubuhi..
Karibuni sana hapa www.kandiliyetu.com usipitwe!
Ukumbi wa mlimani City unavyoonekana kabla ya wajumbe kuingia:


Note: Only a member of this blog may post a comment.