Zoezi la kura
za maoni katika vyama mbalimbali vya siasa hususan Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kuchagua watakaopeperusha bendera kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia
kufanyika Oktoba 25, mwaka huu limezusha vurugu nchini nzima.
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema sehemu mbalimbali kama vile Kiteto, mkoani Manyara, jijini Dar es Salaam, mkoani Mara, Dodoma, Mtwara, Mbeya na Ruvuma wakati wa zoezi hilo kulikuwa na vurugu katika baadhi ya maeneo.
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema sehemu mbalimbali kama vile Kiteto, mkoani Manyara, jijini Dar es Salaam, mkoani Mara, Dodoma, Mtwara, Mbeya na Ruvuma wakati wa zoezi hilo kulikuwa na vurugu katika baadhi ya maeneo.
Jijini Dar watu watano wafuasi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), walinusurika kuuawa na wenzao kwa madai kwamba
walikuwa wakimfanyia kampeni mtu ambaye hawakumtaka.
Tukio
hilo lilitokea mwishoni mwa wiki katika pori la katikati ya Msongola
na Mvuti nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam saa mbili usiku baada ya
watu wasiojulikana kuwavamia wenzao waliokuwa katika pilikapilika za
kujiandaa na kura za maoni za wawania ubunge na udiwani kwa upande wa
CCM.
Akisimulia jinsi tukio hilo lilivyowakuta mmoja wa watu hao aliyeomba jina lake kuhifadhiwa kwa sababu za kiusalama alisema kuwa, wao walikuwa wakitokea Kata ya Zingiziwa Chanika ambako kulikuwa na mkutano wa mgombea wanayemuunga mkono (jina linahifadhiwa).
Akisimulia jinsi tukio hilo lilivyowakuta mmoja wa watu hao aliyeomba jina lake kuhifadhiwa kwa sababu za kiusalama alisema kuwa, wao walikuwa wakitokea Kata ya Zingiziwa Chanika ambako kulikuwa na mkutano wa mgombea wanayemuunga mkono (jina linahifadhiwa).
Alisema kuwa baada ya kutoka kwenye
mkutano huo, walitangulia Mvuti ambako mgombea wao huyo alikuwa amepanga
akutane na wapiga kura wake.
“Si
unajua mikutano kama hii tunatangulia kwanza wapambe ili kuweka mambo
sawa na kuwafanya wale wanaosubiri wawe na imani ya ujio wa mgombea,
tukachukua gari letu aina ya Noah na kuelekea huko tukiwa kumi na mbili.
“Tukiwa tunakaribia kufika tukapigiwa
simu na mtu ambaye hatukumfahamu, akatueleza kuwa tugeuze turudi haraka
sana kwani kuna wapambe wanakuja kutufanyia fujo.
“Walitufanyia vitendo vya kinyama kwa
sababu akina mama tuliokuwa nao waliwavua nguo za ndani na kuwafanyia
vitendo vya udhalilishaji,” alisema kada huyo wa CCM.
Naye
Ditriki Fabiani mmoja wa waathirika hao alikuwa na haya ya kusema: “Kwa
kweli tumepigwa sana bahati ni kuwa kuna wenzetu watatu waliruka na
kukimbilia Kituo cha Polisi Mvuti kutoa taarifa. Wale jamaa siyo watu
kwani hata gari letu licha ya kuvunja vioo walitoa upepo, wakatoweka.”
Alisema baada ya hapo walienda kwa mwenyekiti wa serekali ya mtaa ambaye aliwapigia simu polisi nao wakafika na wakapelekwa Kituo cha Polisi Sitakishari ambako waliandikisha maelezo.
Alisema baada ya hapo walienda kwa mwenyekiti wa serekali ya mtaa ambaye aliwapigia simu polisi nao wakafika na wakapelekwa Kituo cha Polisi Sitakishari ambako waliandikisha maelezo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi,
Ilala SACP Lucas Mkondya alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema
kuwa mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na vurugu hizo.
Huko
Kiteto, Manyara mwandishi wetu ameripoti kuwa Ofisi ya CCM ya Wilaya
ililazimika kufungwa mwishoni mwa wiki baada ya kutokea vurugu kubwa
kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni upendeleo wa baadhi ya wagombea.
Vijana
kadhaa wenye asili ya Kimasai wanachama wa CCM walivamia ofisi hiyo kwa
madai kuwa walikuwa wakikataliwa kupiga kura ya maoni mpaka wawe na
kadi mbili, ya CCM na ya mpiga kura inayotolewa na tume ya uchaguzi.
Ilibidi polisi wafike na kuwakamata
vijana hao waliodai kuwa hawakuwa na hatia kwa sababu wasimamizi wa kura
walitaka kupindisha kanuni za chama.
Vurugu
zingine zilitokea Tarime, Mara kwa madai kuwa kuna baadhi ya wagombea
wapambe wao walikuwa na kura ambazo zilipigwa tayari.
Waliohusishwa na tukio hilo na kukanusha kuhusika ni Gaudensia Kabaka na Nyambari Nyangwine.
Hadi
juzi baadhi ya walioshinda kura za maoni kwa upande wa CCM ni Peter
Serukamba Jimbo la Kigoma Mjini, Jonister Mhagama wa Songea aliyepita
bila kupingwa Jimbo la Peramiho, Philimen Mollel wa Jimbo la Arusha
alikuwa anaongoza.
Nape Nnauye wa Jimbo la Mtama aliongoza
na Dk. Harrison Mwakyembe aliongoza Kyela. Kinondoni Idd Azam aliongoza
na Korogwe Mjini, Mary Chitanda alikuwa anaongoza.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Steven Kabwe alipita bila kupingwa Jimbo la Serengeti.

Note: Only a member of this blog may post a comment.