Na Gregory Nyankaira, Mara
BIBI kizee Selina Akeyo (60), mkazi wa Buembu, nchini Kenya amenusurika kuuawa kwa kucharangwa mapanga na kijana wa marehemu Daniel Okumbo (72) baada ya kutuhumiwa kumuua kwa kumuwekea sumu kwenye pombe aina ya gongo. Tukio la kuwekewa sumu Daniel Okumbo, mkazi wa Kijiji cha Ikoma, wilayani Rorya Mkoa wa Mara inadaiwa lilitokea kijijini hapo Julai 25, mwaka huu.
Walioshuhudia tukio hilo wamedai kwamba, bibi kizee huyo alikuwa akiishi na hawara yake huyo nyumbani kwake Buembu, Kenya kwa miaka kadhaa baada ya mzee Okumbo kufiwa na mkewe.
Imedaiwa kuwa, bibi kizee huyo alichukua uamuzi wa kumuua mpenzi wake baada ya kukasirishwa na kitendo cha mtoto wa kiume wa Okumbo kumjengea nyumba baba yake katika Kijiji cha Ikoma kinachopakana na Buembu kisha kumfuata baba yake kutoka kwa bibi kizee huyo na kumpeleka kuishi katika nyumba yake hiyo.
“Baada ya Okumbo kurudishwa na kijana wake nyumbani Julai 20, mwaka huu, siku iliyofuata bibi kizee huyo alimfuata mzee Okumbo akiwa na chupa ya gongo na alipofika alimpa.
“Watoto wanaamini kuwa gongo ile ilikuwa na sumu kwa sababu baada ya kuinywa akaanza kuumwa tumbo kisha akamuita kijana wake Nyabhaloma Okumbo (36) ambaye alimkuta akigaragara kitandani akamueleza sababu ni gongo iliyoletwa na mwanamke huyo, kisha akakata roho,” kilisema chanzo.
Naye kijana Nyabhaloma Okumbo alikiri kutokea kwa tukio hilo akasema wakati akitafakari afanyeje ili ampeleke baba yake zahanati, ghafla akafariki jambo lililosababisha aangue kilio na kukimbilia panga ili amcharange yule bibi.
“Majirani waliniwahi na sikufanya nililokusudia kwa sababu namhusisha na kifo cha baba yangu ambaye kabla ya kunywa gongo alikuwa mzima wa afya,” alisema kijana huyo.
Aliongeza kuwa ameshindwa kumpeleka bibi kizee huyo kwenye vyombo vya sheria kwani wakati wakiwa katika harakati za kumzika baba yao alitoweka na sasa yupo nchini Kenya.
‘Nilitaka nimfikishe huyo bibi mahakamani kwa kumuua baba, lakini nimeshindwa kwa vile anaishi nchi nyingine na mimi sitaki usumbufu wa kesi na badala yake wana ukoo tumekubaliana kuwa tunaendelea na mambo ya kimila

Note: Only a member of this blog may post a comment.