Wednesday, August 19, 2015

Anonymous

Kocha wa SIMBA SC Awabadilikia MGOSI, KAZIMOTO!

o7bkHdw7
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
KATIKA kuhakikisha timu yake inapata matokeo mazuri kwenye mechi zake, Kocha Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amesema kuwa atapanga kikosi chake cha kwanza kulingana na uwezo wa mchezaji na siyo ukubwa wa jina la mchezaji.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA ya Uganda iliyochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambayo ilimalizika kwa Simba kushinda mabao 2-1.

Miongoni mwa wachezaji mastaa ambao Simba imewasajili ni Mussa Mgosi aliyetokea Mtibwa Sugar, Mwinyi Kazimoto wa Al Markhiya ya Qatar na Hamis Kiiza aliyeichezea Yanga msimu uliopita.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kerr alisema kikubwa anataka kuona kila mchezaji anatimiza majukumu yake ndani ya uwanja ili timu ipate ushindi na hatimaye kutwaa ubingwa wa ligi.

Kerr alisema, hataki kumpanga mchezaji kwa kumfurahisha na badala yake anatakiwa kuisaidia timu huku akisisitiza katika hilo atahakikisha analisimamia ili kutengeneza nidhamu ya timu.

Aliongeza kuwa, katika kikosi anafurahishwa na uwezo wa kila mchezaji licha ya safu ya ushambuliaji kuwa na upungufu na inatakiwa kuboreshwa kwa kusajili mshambuliaji mwingine mwenye uwezo mkubwa atakayesaidiana na akina Mgosi na Kiiza.

“Kila mchezaji anatakiwa kutambua wajibu wake wa ndani ya uwanja kwa kuanza nimewaambia wachezaji wangu kuwa nitampa mchezaji nafasi ya kucheza kulingana na uwezo, mchango wake katika timu na siyo ukubwa na umaarufu wake.

“Hata kama mchezaji akiwa na ukubwa wa jina vipi, kamwe sitampa nafasi ya kucheza katika timu, ili timu ipate ushindi lazima kila mchezaji atimize majukumu nitakayompa kabla ya mechi.
“Haiwezekani kabisa mchezaji apate nafasi ya kucheza wakati hana msaada, kisa tu ana jina kubwa,” alisema Kerr.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.