Khadija Mngwai, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limefunguka kwa kusema kuwa, litazuia usajili wa wachezaji wapya wa timu zote za ligi kuu zikiwemo timu za Simba na Yanga kufuatia madeni ya wachezaji wanaowadai baada ya kuwaacha.
Timu ya Simba ndiyo inayoongoza kwa madeni kufuatia kudaiwa na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Amissi Tambwe na Pierre Kwizera dola 10,000 kila mmoja, Haruna Chanongo shilingi milioni 10 na Donald Musoti dola 13,800, ambaye kesi yake ya madai ipo Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Hadi sasa Simba imeshasajili wachezaji kadhaa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara akiwemo Mussa Hassan Mgosi, Hamisi Kiiza, Peter Mwalyanzi, Vincent Agban, Justice Majabvi na Emilly Namubona.
Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine, amefafanua kuwa kwa timu zote za ligi kuu zikiwemo timu kongwe za Simba na Yanga iwapo hazijakamilisha malipo ya wachezaji ambao wamewavunjia mikataba bila ya kuwalipa stahiki zao, watalazimika kuzuia usajili wao mpya hadi pale malipo yatakapofanyika.
“Nianze kwa kutoa rai kwa timu zote za ligi kuu kuhakikisha zinamalizana na wachezaji wao wote waliowaacha kwa lengo la kupata fursa ya kusajili wachezaji wengine kujaza nafasi hizo.
“Klabu zijue kwamba, iwapo kutakuwa na madai ya wachezaji wa zamani ambao hawajalipwa haki zao, basi zinaweza kuwagharimu katika usajili wao mpya labda wawe wamemaliza kuwalipa madeni yao ama wawe kwenye hatua nzuri ya kufanya mazungumzo ya mwisho ya kuwalipa.
“Safari hii tutakuwa makini kwa kuhakikisha wachezaji wote wanalipwa haki zao kwa mujibu wa sheria, ndiyo maana tumeamua kutumia njia hii ya usajili kwa majina yatakayowakilishwa hapo baadaye,” alisema Mwesigwa.
Aidha, kwa upande wa Yanga wachezaji ambao wamepeleka madai yao katika Chama cha Wachezaji Soka Tanzania (Sputanza) ni pamoja na Jerry Tegete, Danny Mrwanda na Said Bahanuzi anayedai kiasi cha shilingi milioni saba kufuatia kukatishwa kwa mikataba yao bila ya malipo.
Hii ina maana kuwa kama TFF watashikilia msimamo wao, basi watazuia usajili wa Donald Ngoma, Deus Kaseke, Geofrey Mwashiuya na Vincent Bossou.
Hata hivyo alipoulizwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, kuhusiana na hilo alisema: “Sisi hatudaiwi na wachezaji hao, kwa kuwa tuliwaacha kwa taratibu za sheria za soka.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.