Wednesday, August 19, 2015

Anonymous

Kamusoko amtia jeuri Tambwe dhidi ya Azam

AmissTambwe2.jpgSweetbert Lukonge na Wilbert Molandi
MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa Burundi, Amissi Tambwe, ametamba kuwa timu hiyo itafanya vizuri katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC itakayofanyika Jumamosi.
Tambwe amepata jeuri hiyo baada ya kudai kuwa kikosi cha Yanga hivi sasa kipo vizuri kutokana na kuimarika kwa safu yake ya kiungo inayoundwa na nyota kadhaa, akiwemo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko, aliyetua klabuni hapo hivi karibuni akitokea FC Platinum ya Zimbabwe. Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema ujio wa Kamusoko klabuni hapo umeongeza chachu ya ushindi kwani ameonekana kuwa na msaada mkubwa katika kikosi. Alisema uwezo wake wa kuanzisha mashambulizi kwa kupiga pasi za uhakika, ndiyo jambo linalomfanya aamini kuwa Yanga itaisambaratisha Azam siku hiyo ya Jumamosi katika mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Mechi yetu ya Jumamosi dhidi ya Azam itakuwa ni ngumu, lakini nina matumaini kuwa tutaibuka na ushindi kutokana na maandalizi tuliyofanya mkoani Mbeya. “Pia ubora wa safu yetu ya kiungo kwa sasa nayo ni moja ya mambo yanayonifanya niamini kuwa, hilo linawezekana kwani tangu Kamusoko aliposajiliwa, ameongeza chachu ya ushindi kwa sababu ana uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi ya aina yote yakiwemo yale ya kushtukiza,” alisema Tambwe ambaye alijiunga na timu hiyo msimu uliopita akitokea Simba.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.