UCHUMBA wa muda mrefu wa Mtangazaji wa
Runinga ya Clouds, Ben Kinyaiya na mpenzi wake, Suzy aishiye nchini
Uingereza, umeingia shubiri baada ya msanii huyo kudaiwa ‘kuruka ngome’
na kupata mtoto na mwanamke mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Nasra.
“Unajua Ben alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine hapa Bongo (Nasra) tofauti na huyo wa Uingereza (Suzy) na katika uhusiano wao, walipata mtoto wa kike anayeitwa Nilla na Suzy alipogundua hivyo, aliamua kukata uhusiano na Ben, hali iliyosababisha aende Uingereza kubembeleza,” kilisema chanzo.
Amani lilimvutia waya Ben ambaye alisema hataki kuingiliwa kwenye mambo yake binafsi.


Note: Only a member of this blog may post a comment.