Muimbaji wa Marekani, Taylor Swift anadaiwa kuipiga chini dili ya
kutumbuiza nyimbo 3 tu kwenye harusi ya bilionea mmoja, ambayo
ingemuingizia dola milioni 2, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 4.
“You have to admire her for putting friendship ahead of financial considerations. She said no to a small fortune so she could bring happiness to a good friend.” – mmoja wa waliohudhuria sherehe hiyo aliliambia gazeti la Sunday Express.
Taylor alihudhuria sherehe hiyo akiwa na boyfriend wake Calvin Harris.
Taylor na Calvin mwaka huu walitajwa na jarida la Forbes kuwa couple maarufu iliyoingiza fedha nyingi zaidi mwaka 2015, na kuwazidi Jay Z na Beyonce waliokuwa wamekamata nafasi hiyo mwaka uliopita. Kwa pamoja waliingiza dola milioni 146.
Hii inaonesha kuwa Taylor hana njaa, na huenda hiyo ni sababu ya kuamua kumjali rafiki yake badala ya dola milioni 2 za bilionea aliyemtaka akatumbuize kwenye harusi yake kwa muda mfupi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.