Friday, August 21, 2015

Anonymous

IMEFAHAMIKA! Hii Ndio Sababu Iliyoifanya TAIFA STARS Kufuta Mpango wa Kwenda Oman!

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa August 22 ilikuwa iende Oman kucheza mechi moja ya kirafiki na timu ya taifa ya nchi hiyo kabla ya kwenda Instabul Uturuki kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya michuano ya kuwania kupata tiketi ya kucheza michuano ya AFCON 2017.
DSC_0022
Stars ambayo inajiandaa na mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles mchezo utakaochezwa Septemba 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam imefuta safari hiyo baada ya Oman kushindwa kukizi vigezo vya FIFA vya kuandaa mechi za kimataifa za kirafiki.
DSC_0030
Hivyo Taifa Stars itaondoka Dar Es Salaam August 23 kuelekea moja kwa moja Instabul Uturuki na mpango wa kwenda Oman umekufa tena, Stars itaweka kambi ya siku nane kabla ya kurejea Dar Es Salaam kuwa subiri wageni wao Nigeria Super Eagles, huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa Stars baada ya ule wa kwanza kufungwa 3-0 na Misri.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.