Staa wa Bongo Fleva, Aunt Ezekiel.
ISHU! Katika kitu kinachoweza
kutafsiriwa kama kituko, wasanii wawili wanaofanya vizuri kwenye filamu
na Bongo Fleva, Aunt Ezekiel na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ juzikati
walionekana wakijishebedua na wapenzi wao wanaotajwa kuwa ‘majanki’
kuliko wao, mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya fainali ya
Kinondoni Talent Search, iliyofanyika katika ukumbi wa Kisanga,
Millenium Tower, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wawili hao walitinga ukumbini hapo wakiwa na wapenzi wao hao na kukaa pamoja huku wakipigana vibega kama ilivyo kawaida ya wapenzi, kiasi cha kuwaacha watu midomo wazi, hasa kwa kuzingatia kuwa ndani ya ukumbi huo kulikuwa na ugeni mkubwa.
Wakiwa kwenye fainali hizo zilizoratibiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, Aunt na Shilole muda mwingi walionekana wakichezacheza na mabwana zao hao, Mose Iyobo na Nuh Mziwanda.
“Dah angalia Shilole na Nuh wake wanavyojishebedua mbele ya JK utadhania wao ndiyo wageni rasmi vile, halafu hali hiyo pia nimeiona kwa Aunt na Mose Iyobo na wao wamekaa kule nyuma lakini muda wote ni kunong’onezana na kucheka tu na hawaachani utafikiri wamekuja kutangaza mapenzi na ndoa zao humu,” alisema mmoja wa mashuhuda.

Note: Only a member of this blog may post a comment.