Brighton Masalu
SIKU chache baada ya gazeti dada
ya hili la Ijumaa Wikienda kuripoti juu ya wazazi wa Jokate Urban
Mwegelo ‘Kidoti’ kumkataa Ali Kiba kama mchumba wake, binti huyo
ameibuka na kuwataka wazazi kote nchini kuacha kuwaingilia watoto wao
katika masuala ya kimapenzi, akidai jambo hilo ni vema wakiachiwa
wenyewe.
Akizungumza
na gazeti hili, Jokate alisema ni vyema kama wazazi wakawaacha watoto
wao waoe au kuolewa na watu wawapendao, kwani vinginevyo ni kuwaingilia
maisha na uhuru wao binafsi, jambo ambalo si jema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.