Kundi la Navy Kenzo limeanza kuyaona matunda ya kufanya kazi na
Vanessa Mdee ambaye tayari amejitengenezea connection nyingi nchini
Nigeria na Afrika kwa ujumla.
Baada ya kuchia video kali iliyoongozwa na director wa Afrika Kusini,
Justin Campos wimbo wao ‘Game’ ambao wamemshirikisha Vanessa, tayari
umeanza kufanya vizuri kwenye chati za muziki za vituo vya Nigeria.
Wiki hii (August 21) wimbo huo umekamata namba 1 kwenye African Top
10 ya kituo kikubwa cha Radio cha Nigeria, The Beat 99.9Fm.
Mtanzania mwingine ambaye yumo kwenye chati ya wiki hii ya kituo
hicho ni Alikiba, ambaye wimbo wake ‘Chekecha Cheketua’ umekamata nafasi
ya 9.
African Top 10 huwa inasikika kila Ijumaa kupitia kipindi cha Morning Rush cha The Beat 99.9 Fm ya Lagos, Nigeria.

Note: Only a member of this blog may post a comment.