Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media, Rhys akizungumza jambo katika hafla hiyo.
KAMPUNI ya Azam Media Group Ltd inayokua kwa kasi kubwa nchini imezidi kuboresha huduma zake kupitia king’amuzi chake cha Azam TV baada ya jana kuzindua chaneli mpya ya Azam Sports HD yenye ubora wa hali ya juu wa picha (ung’avu wa picha).
Zaidi ya hapo, pia imetangaza ujio rasmi wa Ligi Kuu Hispania, La Liga ambayo itakuwa ikionyeshwa ‘live’ kupitia chaneli hiyo mpya inayopatikana katika vifurushi vyote vya Azam TV kwa malipo ya nyongeza ya Sh 15,000 tu kwa mwezi.
Kwa Tanzania, La Liga ndiyo ligi pendwa baada ya Ligi Kuu England (EPL), huku mechi ya mahasimu wa ligi hiyo kati ya Barcelona na Real Madrid, maarufu kama El Classico zitakuwa zikionyeshwa moja kwa moja na kuchambuliwa kwa kina kabla, wakati wa mapumziko na baada ya mchezo na timu nzima ikiongozwa na gwiji Charles Nkwanga Hilaly.
Akizungumza katika ofisi za Azam TV zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam, ambapo hafla hiyo imefanyika, Ofisa Mtendaji wa Azam Media, Rhys Torrington amesema kuwa ni furaha kubwa kwa kampuni yao kupiga hatua ya kuonesha moja ya ligi kubwa duniani na kuweka bayana kuwa kazi itaanza rasmi Ijumaa Agosti 21, mwaka huu na mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo utakuwa kati ya Sevilla dhidi ya Malaga.
Alisema kuwa mbali na La Liga, pia uhondo wa Ligi Kuu Bara (VPL) utaendelea kama kawaida ambapo umeboreshwa katika muonekano wa HD kwa wale wenye runinga zenye uwezo huo, hata hivyo kwa wasio na runinga hizo wataendelea kufaidika lakini siyo katika kiwango cha HD.
“Uzinduzi wa Azam Sports HD ni hatua kubwa katika maendeleo ya Azam TV, tumejipanga kukidhi mahitaji ya teknolojia kwa ajili ya kutoa picha zenye ubora wa HD, jambo ambalo hatukutazamia tungelitekeleza ndani ya muda mfupi namna hii na hatua ya kuwezesha kurusha mechi za La Liga ni jambo kubwa zaidi,” alisema Torrington.
Amesema kuwa huduma ya Azam Sport HD itapatikana Tanzania tu na huduma ya Sport HD inapatikana katika aina zote za vifurushi kwa nyongeza ya Sh 15,000 kwa mwezi.
Aidha katika hafla hiyo alitambulisha timu nzima ya watangazaji inayoundwa na Charles Hilaly (mkuu wa kitengo), Baruan Muhuza, Patrick Nyembera, Twalib Omary na wengineo huku kwa upande wa timu ya wachambuzi ikiundwa na Ally Mayay, Edo Kumwembe, Kally Ongalla, Jeff Leah na wengine.

PICHA/STORI: MUSA MATEJA NA DENIS MTIMA/GPL
Note: Only a member of this blog may post a comment.