Monday, August 3, 2015

Anonymous

10 PICHAZ: Hivi ndivyo ilivyokuwa ndoa ya wakala wa RONALDO, mastaa kibao waliohudhuria!

Hatimaye wakala namba moja wa wanasoka bora ulimwenguni, Jorge Mendes jana alifunga ndoa na mchumba wake wa siku, Sandra Barbosa.
 
Sherehe ya ndoa ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa soka ulimwenguni, huku Cristiano Ronaldo, mteja mkuu wa Mendes akiwa ‘mpambe rasmi’ wa bwana harusi.
Cristiano Ronaldo akiingia kanisani
Wageni waalikwa wengine walikuwa ni kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson, Raisi wa Real Madrid, Florentino Perez, James Rodriguez, Jose Bosingwa na Deco De Souza pamoja na Pepe.
Mwanasoka Pepe wa Real Madrid nae alikuwepo 
Mchezaji wa zamani wa Chelsea na Barcelona Deco De Souza 
James Rodriguez wa Real Madrid nae alihudhuria 
Bwana Harusi Jorge Mendes 
Jose Bosingwa – mchezaji wa zamani wa Chelsea
Rais wa Real Madrid Florentino Perez
   

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.