Wednesday, July 15, 2015

Anonymous

YANGA SC Yajichimbia Jeshini Dar

WAKIJIANDAA na michuano ya Kombe la Kagame, Yanga wameamua kufanya mazoezi yao kwa kificho kikubwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.
DSC00287 Uwanja huo wanaoutumia Yanga kufanya maandalizi hayo, unamilikiwa na Jeshi la Polisi ambao umekuwa ukitumiwa na  timu za majeshi zinazojiandaa na michuano mbalimbali.

Timu hiyo, ilianza kufanya mazoezi yake kwa mara ya kwanza jana Jumanne ikitokea Uwanja wa Karume waliokuwa wanautumia awali kabla ya kuhama.
Championi Jumatano, lilifika kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuripoti taarifa za timu hiyo, lakini lilishindwa kufanikiwa kuingia ndani baada ya kuzuiliwa getini na maofisa wa polisi hao.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Michezo wa Jeshi na Mkurugenzi Msaidizi wa Ulinzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Inspekta Mohammed Manyai, alisema kuwa Yanga wamewataka kumzuia mtu yeyote kuingia kwenye mazoezi hayo.
Manyai alisema, kwa mujibu wa benchi la ufundi la timu hilo chini ya Kocha Mkuu Mholanzi, Hans van Der Pluijm, hivi sasa mazoezi wanayoyafanya ni ya kimbinu, hivyo hawataki kuyaonyesha kwa watu kwa hofu ya wapinzani wao kujua wanachofanya.
 DSC00288“Sisi kama jeshi hatuwezi kuwazuia kwenda kuangalia na kuripoti mazoezi ya Yanga, lakini kikubwa Yanga wenyewe ndiyo wamezuia waandishi na watu wengine kuingia uwanjani kutazama mazoezi yao.

“Kikubwa Yanga wamezuia mazoezi yao yasiangaliwe na watu kwa ajili ya kuwaongezea umakini wachezaji wao kwa hofu ya kelele za mashabiki, pia kuficha mbinu zao wanazozitumia hivi sasa,” alisema. Yanga wameanza mazoezi leo (jana) asubuhi wenyewe watakuwa wanapishana na timu ya Kombaini ya Majeshi kila siku uwanjani; kila moja ikijiandaa na michuano yake.
Championi lilishuhudia ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa kwenye kambi hiyo na kila mmoja aliyekuwa anataka kuingia alikuwa akihojiwa na kama siyo mhusika alikuwa akizuiwa.

“Yanga watakuwa wanaanza mazoezi saa 2:30 hadi saa 5:00 asubuhi mara baada ya timu ya Kombaini ya Majeshi kumaliza mazoezi yake saa 2:00, asubuhi ambayo inaanza saa 12:00 asubuhi. “Wanapishana tena jioni kwa Kombaini ya Majeshi kuanza saa 8:00 mchana na kumaliza saa 10:00, kabla ya Yanga kuingia uwanjani kuanza mazoezi hayo saa 10:30 jioni hadi saa 12:00 jioni kisha kurudi kambini kwao huko Baraza la Maaskofu nyuma ya uwanja huo,” alisema Manyai.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.