Thursday, July 2, 2015

Anonymous

UTATA! Msanii Dayna asema cover ya wimbo wake ‘Nitulize’ imemletea shida!

Dayna Nyange amekiri kuwa cover la wimbo wake ‘Nitulize’ akiwa na Nay wa Mitego lilimletea shida kutokana na kuchukuliwa na jamii kama sio mtu wa aina hiyo.
Dayna Nyange feat Nay Wa Mitego - 'Nitulize'
Dayna ameiambia Bongo5 kuwa kama wazazi wake wangeona cover ya wimbo huo, wangejisikia vibaya kwakuwa ni watu wadini.
“Unajua muziki unatufanya tufanye vitu fulani kwaajili ya muziki na mashabiki wetu. Lakini tunaporudi kwenye maisha ya kawaida mimi ni mtu mwenye kujali maadili,” amesema Dayna. 

“Sema kwenye issue ya cover ya wimbo ‘Nitulize’ iliniletea shida kwa baadhi ya watu na nafikiri zile picha zingewafika wazazi wangu ingekuwa tatizo kidogo, lakini ndo hivyo sio watu wa kwenye social network. Pia mimi ni mtoto wa kiislamu lazima nizingatie kujistili kwenye kazi zangu. Hata ujio wa video yangu utazingatia masuala ya kujistili,” aliongeza Dayna.
Amesema video ya wimbo huo itatoka baada ya mwezi wa Ramadhan.
-via bongo5

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.