Alikiba ameungana na mshindi wa tuzo za Oscar raia wa Kenya, Lupita Nyong’o kwenye kampeni dhidi ya ujangili hasa wa tembo.
Lupita na Alikiba wote ni mabalozi wa taasisi ya WildAid inayoendesha
kampeni ya kuhamasisha watu kuacha kununua bidhaa zitokanazo na ndovu.
Mastaa hao jana walikutana kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Nairobi Kenya ambao wote walihutubia.
Hitmaker huyo wa Chekecha Cheketua aliungana na familia ya Lupita
aliyejizoelea umaarufu kwa kuigiza kwenye filamu ya ’12 Years A Slave’,
kubadilishana mawili matatu.
Alikiba ameshare picha kwenye Instagram ya Lupita akiongea na
waandishi wa habari na kuandika, “WildAid Press Conference Nairobi Kenya
@lupitanyongo gracefully and passionately making a statement for a
positive change in Elephant poaching.”
Kwenye picha nyingine Kiba ameandika: WildAid Press Conference
Nairobi Kenya Nilijiunga Na @lupitanyongo Katika Zoezi La Kutokomeza
Ujangili Wa Tembo.”
“Nikikutana Na Mama Dorothy Nyong’o Na Kukubaliana Kufanya Kazi
Pamoja Kuaangamiza Ujangili Wa Tembo,” ameandika kwenye picha nyingine.
Naye Lupita Nyong’o alipost picha hiyo juu kwenye Instagram na kuandika:
Elephants can hear more than 5km away. So my whisper must be like a
shout at this distance…? #dubiouslogic. Tonight’s gala at
@villarosakempin is to raise funds and awareness to ensure that we get
to hear from elephants for a long long time. @wildaid #ivoryfree
#LNhomecoming #elephants #secretsthatcanbeheard.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.